Jumapili , 13th Jul , 2014

Msanii mahiri wa muziki wa Bongofleva, Baucha hivi sasa anaendeleza kuutangaza muziki wake kimataifa zaidi baada ya kutoa kichupa cha wimbo wake mpya unaoitwa 'Champododo'.

Msanii wa muziki nchini Tanzania Baucha

Baucha ameiambia eNewz kuwa hii ni moja ya kazi yake ya tatu mpya kutoa ambapo mpango mzima unaofuata ni kufanya remix ya ngoma hiyo akishirikiana na msanii Tekno kutoka nchini Nigeria na kuifanyia shooting nchini Italia mwezi Septemba mwaka huu.

Aidha, Baucha ambaye pia huinua vipaji vya wasanii chipukizi ameongezea kuwa ndani ya mwezi huu anatarajia kuibua msanii chipukizi mkali wa miondoko ya hip hop katika lebo yake ya 'Baucha Records'.