Jumatano , 23rd Oct , 2019

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva na mchekeshaji, Whozu amewajibu wanaodai kuwa hana pesa na kudandia kwa ndugu ili kuendelea kuishi mjini.

Whozu

Whozu amesema kwamba maisha yake hapendi kuyaweka sana mtandaoni kwahiyo hakuna haja ya kila mtu kujua anachokifanya lakini ukweli anao yeye na vitu anavyomiliki vina thamani kubwa. 

"Simzuii mtu kuniongelea vibaya, ninaangalia maisha yangu. Hii cheni hapa ni kodi ya mtu kabisa tena ni ya miezi sita au mwaka mzima", amesema Whozu.

"Ninachoweza kusema ni kwamba watu waangalie na kusapoti kazi zangu tu kama mwanzo. Kuhusu hela zangu mimi sichezei, ninafanya vitu vya msingi", ameongeza.

Whozu anatamba na wimbo wa Doko huku pia akishirikishwa katika wimbo wa Sensema wa Hamisa Mobetto ambao umechiwa hivi karibuni.