
Chidi Benz
Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh 38,638, bangi yenye tahamani ya sh 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Awali Februari 18 Chidi Benz alikiri mbele ya Hakimu Mkazi, Waliarwande Lema mashtaka matatu yanayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ya kukutwa na dawa za kulevya, kifuu cha nazi na kijiko vinavyotumika kuvutia ama kunusa dawa hizo za kulevya.
Rapa huyo amefanikiwa kulipa faini hiyo ya shilingi laki 9, na kuachiwa huru baada ya mama yake mzazi kuilipa.