Jumatatu , 8th Jan , 2018

Msanii wa Hip Hop nchini Rashid Makwiro 'Chid Benz anashikiliwa tena  na jeshi la polisi mkoani Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya na hii inakuwa mara ya tatu kwa msanii huyu kukumbwa na sakata hili.

Akithibitisha taarifa hizo Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP, Giless Muroto amesema kwamba ni kweli msanii huyo alikamatwa na taarifa kamili zitatolewa hapo kesho.

Kamanda Muroto amesema "Ni kweli Chidi Benz mnamo tar 30/12/2017, tulimkamata akiwa yeye na mke wake na vijana wawili. Tumemkamata akiwa na dawa za kulevya zinazodhaniwa kuwa ni Heroine. jalada lake lipo tayari kwa Mwanasheria wa wa serikali linafanyiwa uchunguzi na muda wowote watapelekwa mahakamani"

Aidha ameongza kuwa watuhumiwa wote bado wako mahabusu.

Msikilize hapa chini Kamanda Muroto akifafanua zaidi