"Chin Bees ananitafuta, aje nimuoneshe" - Country

Jumanne , 9th Jul , 2019

Wakali wa muziki wa Trap bongo, Chin Bees na Country Boy wameendelea kuvimbiana katika 'Interviews' huku kila mmoja akijipiga kifua kwamba ni bora.

Chin Bees na Country Boy

Zogo hilo limefika hadi katika meza ya eNewz, baada ya Chin Bees kusema kuwa Country Boy hafikii levo zake kwa sasa na kwamba anapaswa ajilinganishe na wasanii wachanga wa Trap bongo, Country Boy amejibu mashambulizi hayo.

Country Boy 'Wiz' amesema, "Chin Bees ana tatizo na mimi, ananitafuta kwa sababu nafanya kazi ambazo zinaonekana zinamgusa, ni mdogo wangu nimemsaidia mimi katika 'game', hanifikii kwa kurap, kuvaa hata maisha", amesema Country Boy.

Pia Country Boy amesema kuwa alihusika katika kumsaidia Chin Bees kwenye kutambulisha ngoma yake ya kwanza.

Tazama hapa majigambo ya wote wawili.