Ijumaa , 9th Mei , 2014

Msanii wa muziki wa dansi, Christian Bella amesema kuwa, kuna haja kubwa ya wasanii kuleta mabadiliko na mapinduzi katika tungo za nyimbo zao, na kuwekeza nguvu zaidi katika kuandika ujumbe ambao unaleta maana zaidi kwa mashabiki.

Christian Bella

Christian Bella amewataka wasanii hawa kujifunza hili katika ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina "Mama", ambayo ataiachia hivi karibuni.

Christian Bella amesema kuwa, amejaribu kuja na kazi ambayo ina ujumbe wa tofauti zaidi na pia ameamua kuchanganya ladha kwa kumshirikisha msanii wa Bongo Flava Ommy Dimpoz katika kazi hii, na hapa anaeleza mwenyewe vizuri zaidi.