Alhamisi , 20th Aug , 2015

Mfalme wa masauti staa Christian Bella amesema kuwa hivi sasa anafanya utambulisho mkubwa wa video ya wimbo 'Amerudi' na bendi yake ya Malaika kama zawadi kwa mashabiki wake katika onesho kubwa la muziki kesho jijini Dar es Salaam.

Mfalme wa masauti staa Christian Bella

Bella anayeendelea kushika chati kupitia kazi zake zikiwemo 'Nashindwa', 'Nakuhitaji', na 'Amerudi,' ameongea na eNewz kuwa hivi sasa yupo mbioni kufanya kazi mpya iitwayo 'Namgharamia' na staa wa muziki wa Bongofleva.