Jumanne , 26th Apr , 2016

Mkali wa muziki wa Dansi na Rhumba Tanzania, Christian Bella ameifahamisha eNews juu ya pengo lililoachwa na Papa Wemba, huku akisema ni mwanamuziki aliyeweka heshika katika mziki wa Congo.

Mwanamuziki wa Dance, Christian Bella

Papa Wemba alitangaza vizuri mziki wa DRC kama Rumba music na kuufanya mzuki huo uweze kutambulika dunia nzima, hata hivyo Bella ameendelea kusema ni pengo kubwa sana kumpoteza nguli huyo.

Bela amesema alifanikiwa kufanya naye show na ku-share stage moja mwaka 2008, ambapo alikuja Dar es salaam wakati huo Bella akiwa katika bendi ya Akudo na alipata mda wa kuongea naye mambo mengi

Bella anasema umri wake ulikuwa umesogea, kwa hiyo ni mipango ya Mungu.

Wemba alianguka jukwaani ghafla huko ABIDJAN na kupoteza uhai wake hapo hapo.