Alhamisi , 26th Jun , 2014

Msanii kutoka nchini Jamaica, Christopher Martin anatarajiwa kutua nchini Uganda na kutoa burudani mwezi wa 9 mwaka huu, akiwa pamoja na msanii mwenzake Celil kutoka Jamaica pia.

Wasanii wa nchini Jamaica, Cecile na Christopher Martin

Burudani ya onesho kali kabisa kutoka kwa msanii huyu, itafanyika ndani ya Jiji la Kampala katika tukio ambalo linatarajiwa kupewa sapoti ya kutosha pia na wasanii wakali kabisa wa mindoko ya reggae na dancehall kutoka nchini Uganda.

Christopher Martin ni miongoni mwa mastaa wakali kabisa kuweka rekodi ya kutumbuiza katika jiji la Kampala, akiwa katika orodha hii sambamba na wasanii Sean Paul, Shaggy, Konshens, Sean Kingstone, Mack Diamond, Alaine, Mr. G, Busy Signal, Elephant Man na wengineo.