Chuchu Hansy ataja anachojutia kuwa na Ray

Alhamisi , 26th Mar , 2020

Msanii wa filamu nchini Chuchu Hansy amesema, moja ya vitu anavyojutia kuwa kwenye mapenzi  na baba wa mtoto wake Vicent Kigosi "Ray" ni mahusiano yake kuwa wazi na ku-date na mtu maarufu.

Wasanii wa filamu Chuchu Hansy na Vicent Kigosi "Ray"

Akieleza hayo kupitia show ya Planet Bongo ya East Africa Radio, inayoruka kila siku za Jumatatu - Ijumaa kuanzia 7:00 mchana hadi 10:00 jioni, amesema kama mwanamke anahitaji tuzo maana kudate na mtu maarufu ni shida na anapitia changamoto nyingi.

"Sijawahi kukosana na Baba Jayden, mimi ni mwanamke mwenye historia kwake na hatoweza kutokea mwingine, ila kitu nachojutia kwake ni mahusiano yangu kuwa wazi na kudate na mtu maarufu" amesema Chuchu Hansy.

Pia ameendelea kusema "Napitia changamoto nyingi kama mwanamke, nahitaji tuzo maana ninayopitia ni magumu kama wivu, wanawake kumkumbatia mpenzi wangu, kufuatwa na wanawake wazuri au kum-kiss".