Alhamisi , 31st Jul , 2014

Baada ya kumaliza usaili wake wa pili wa Dance100% 2014 pale Don Bosco Oysterbay Jumamosi, sasa imebaki nafasi moja tu ya mwisho kwa makundi yenye vipaji vya kudansi Tanzania.

mashindano ya kucheza muziki Dance 100% 2014

Makundi hayo kwa pamoja yataingia katika mashindano haya kupitia usaili wa mwisho utakaofanyika Temeke jijini Dar es Salaam, katika viwanja vya TCC Chang'ombe Jumapili tarehe 3 mwezi Agosti.

Mpaka sasa makundi 10 tayari yamekwishapatikana ambapo yanaingia moja kwa moja hatua ya robo fainali ya mashindano haya makubwa nchini Tanzania.

Safari ndiyo inazidi kupamba moto huku wote tukitaka kujua nani atakuwa King wa Dance100% 2014 na kuondoka na kitita cha shilingi milioni Tano za Tanzania.

Kumbuka, Mashindano haya hayana kiingilio chochote.