Jumapili , 20th Jul , 2014

Zoezi la usahili wa mashindano makubwa ya kucheza nchini Tanzania, Dance100% 2014 limeanza kwa kishindo hapo jana katika viwanja vya Don Bosco Upanga Jijini Dar es Salaam kwa kujitokeza kwa vikundi mbalimbali kufanyiwa usaili.

Mashindano ya kucheza ya Dance 100% 2014 jijini Dar es Salaam

Vikundi mbalimbali takribani 17 vimeweza kujitokeza katika usaili huo wa Dance100% ikiwa ni msimu wa tatu na kwa jana ni makundi matano tu yaliyofaulu kufuzu usahili, huo wa kwanza kufanyika kwa mwaka huu.

Safari ndio kwanza imeanza kuelekea katika shindano hili kubwa la kudansi ambalo litashuhudia bingwa wa Dance 100% 2014, akijinyakulia zawadi nono ya kitita cha shilingi milioni tano za Tanzania.