Ijumaa , 5th Sep , 2014

Wapenda Burudani kutoka sehemu mbalimbali za Jiji la Dar wameendelea kuonyesha hamasa na matarajio makubwa tayari kwa kuburudika tamashani siku ya kesho pale Leaders Club.

washindi wa zawadi za tamasha la Kilimanjaro Music tour Leaders Club jumamosi hii.

eNewz ikiambatana na timu ya East Africa Radio, leo imetimba Kinondoni katika baadhi ya maeneo yaliyobakia kufikia nasi na kuongea na kuwazawadia mashabiki ambao wameweza kujibu maswali kuhusiana na tukio hili kubwa.

Kumbuka, shughuli nzima ni kesho, wasanii sio chini ya 14 watatumbuiza juu ya Jukwaa wakiwemo Ommy Dimpoz, Professa Jay, Ben Pol Mwana Fa, AY, Rich Mavoko, Malkia Khadija Kopa, Jamobo Squad, Vanessa Mdee, Christian Bella, Mashujaa Band, Weusi pamoja na Jose Mara na Bendi yake.

Na kiingilio katika onyesho hili ni shilingi 3,000 tu, na unapatiwa kinywaji chako bure mlangoni halafu Tunazungusha Kikwetukwetu.