Jumanne , 18th Feb , 2014

Dayna Nyange, Msanii wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya Mimi na Wewe, baada ya kumaliza ziara yake ya kimuziki huko Kanda ya Ziwa, tayari amerejea jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuendeleza harakati nyingine za maisha na kimuziki.

Dayna katika ziara yake hii, kati ya mambo ambayo yalikuwa ni kivutio kikubwa, ni ukaribu alioujenga na msanii Cindy Sanyu kutoka nchini Uganda, ambapo amesema kwa muda mfupi tu yeye pamoja na msanii huyu wameweza kupatana sana kutengeneza urafiki mkubwa pamoja na kuweka mipango ya kutengeneza colabo ambayo inafikia ngazi za kazi inayotamba kwa sasa kutoka kwa mwanadada Rihanna na Shakira, Remember to Forger You.

Dayna amesema kuwa, Hivi karibuni mambo yakishakaa sawa atasafiri kwenda huko nchini Uganda kwaajili ya kukamilisha mchongo huu wa kutengeneza kolabo na msanii Cindy Sanyu.