Ijumaa , 11th Jul , 2014

Msanii wa kike ambaye anakubalika sana katika muziki wa kizazi kipya nchini Dayna Nyange anatarajia kutoa video ya wimbo wake mpya ambao unatarajiwa kukamilika baada ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

Msanii wa muziki nchini Dayna Nyange

Dayna ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake 'I Do' ameiambia enewz kuwa kwanza anatoa shukrani zake za dhati kwa mashabiki wake kuupokea vyema wimbo wake huo na amewasihi wategemee shooting kali ya wimbo huo.

Dashosti huyo amesema kuwa hii itakuwa ni surprise kubwa sana kwani katika video hiyo mpya amejitahidi kubadilika tofauti na video zake zote alizowahi kufanya hapo awali, ambapo prodyuza mahiri anayeipika kazi hiyo ni Triss kutoka studio maarufu ya Conga Music jijini Dar es Salaam.

Dayna pia ametuma picha zake za kuwatakia mashabiki wake wote mfungo mwema wa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani .