Jumanne , 27th Apr , 2021

Mtangazaji wa kipindi cha Nirvana ya East Africa TV Deogratius Kithama, amelichambua vazi la kijiko,uma na visu vya siagi ambavyo amevaa msanii na CEO wa Konde Music Worldwide Harmonize kwenye video ya wimbo wake wa Attitude.

Kulia ni mtangazaji Deon Kithama, kushoto ni msanii Harmonize

Kwanza Deo Kithama amemsifia msanii huyo kwa kuleta ubunifu mpya wa mavazi kwenye upande wa video kwani haijawahi msanii yeyote wa Bongo kuvaa 'style' ile ya mavazi

"Harmonize ni mtu ambaye anajaribu kila kitu kuanzia muziki na amefanya mabadiliko makubwa sana kwenye tasnia, kwenye ile video amependeza, amevaa nguo zenye rangi ya kisasa, kuhusu vazi la kijiko ameonyesha utofauti mkubwa sana kwa sababu mitindo ni sehemu ya kuonesha utofauti" 

"Vazi lile kwenye fashion halipo ila kwenye style lipo, kama wewe ni msanii lazima uwe na jicho la kisanii ndio maana watu wanamuongelea hivi sasa kwa sababu hatujaona mtu kuvaa vazi la vijiko na uma kama vile, imependeza sana" ameongeza Deo Kithama

Mengine zaidi aliyoyasema Deo Kithama akilichambua vazi hilo bonyeza hapa kutazama.