Jumatatu , 17th Feb , 2014

Msanii wa muziki Diamond Platinumz, amewahakikishia mashabiki wa muziki wake mabadiliko na maendeleo makubwa katika maonyesho yake kwa mwaka 2014 kwa lengo la kuendelea kubaki kileleni na kuzidi kuwavutia mashabiki wake kila siku.

Msanii huyu amesema kuwa kila siku anajitahidi kujituma na kuwa mbunifu ili kuendelea kupata showz zaidi, kitu ambacho pia ni siri pekee ya mafanikio yake.

Diamond amewataka mashabiki wake kutarajia mambo makubwa sana kutoka kwake kwa mwaka huu ambao ana matumaini makubwa kuwa atautumia vizuri kufanya mambo mapya na tofauti.