
Miss Tanga 2014 Diana Festo
Shindano hilo limefanyika kwa mafanikio makubwa katika mchuano mkali kabisa wa warembo 14, ambapo pia mrembo Noon Juma ndiye aliyeshikilia nafasi ya pili, akifuatiwa na Vanessa Charles katika nafasi ya tatu na kutoka Tanga Mkonge Hotel, hivi ndivyo mambo yalivyokuwa.
Shindano hili lililoongozwa vyema na MC, Mtangazaji mahiri wa EATV Deogratius Kithama, lilihudhuriwa na ugeni mzito wa Mkuu wa wilaya ya pangani Hafsa Mtasiwa, kama mgeni rasmi pamoja na kutiwa nakshi na burudani kutoka kwa Malkia wa Mipasho Bi. Khadija Kopa.