
Kwenye ukurasa wake wa twitter, Diddy ameandika ujumbe akisema kwamba kwa siku 3 mfululizo alikuwa akijaribu kuamka katika ndoto mbaya aliyokuwa nayo, kwani alikuwa hajui nini cha kufanya, lakini sasa atajaribu kuelezea mahusiano yao yasiyoelezeka.
“Kwa siku tatu zilizopita nilikuwa nikijaribu kuamka kutoka kwenye ndoto mbaya, lakini nimeshindwa, sijui nitafanya nini bila wewe baby, nakumiss sana. Leo naenda kutoa heshima, naenda kujaribu kutafuta maneno ya kuelezea mahusiano yetu yasiyoelezeka”, aliandika Diddy.
Diddy aliendelea kwa kuandika, "Tulikuwa ni zaidi ya marafiki wa karibu, zaidi ya soul mate, tulikuwa zaidi ya ujinga mwengine, na nakumiss sana."
For the last three days I’ve been trying to wake up out of this nightmare. But I haven’t. I don’t know what I’m going to do without you baby. I miss you so much. Today I’m going to pay tribute to you, I’m going to try and find the words to explain our unexplainable relationship. pic.twitter.com/QtVnUrv0ep
— Diddy (@Diddy) November 18, 2018
Ikumbukwe kwamba Ijumaa ya Wiki iliyopita Diddy alipata msiba mkubwa wa kufiwa na mama watoto wake, mwanamitindo na muigizaji Kim Porter, ambaye aliugua kwa muda mfupi sana.
Kim Porter ameacha watoto wanne, watatu kati yao ambao ni Christian, Dlila, na Jessie amezaa na Didy, huku mmoja anayejulikana kwa jina la Quincy, alimzaa kabla ya kukutana na Diddy, lakini Diddy 'alimuadopt'.
