Diss ya Video ya simu yamuamsha TID

Jumatatu , 13th Mei , 2019

Msanii wa Bongofleva TID amekataa kumzungumzia msanii mwenzake Q Chilla, ambaye alimwambia kuwa video yake kafanya na simu ya mkononi.

Msanii TID

Akiongea kwenye eNewz ya East Africa Television, TID amefunguka kuwa kwasasa anataka kuongelea zaidi muziki wake na hataki kumpa nguvu mtu mwingine.

''Nimekuwepo kwenye game kwa muda mrefu sasa na mtu anayesema muziki wangu mbaya yeye pia hawezi kuwa mzuri kwahiyo ni wivu tu wa hatua nilizopiga muda mrefu kwasababu mimi ni legend'', amefunguka.

TID ameachia ngoma hivi karibuni inaitwa Najidai ambayo amemshirikisha Q Chilla, lakini msanii huyo hakutokea kwenye Video na baadaye aliweka wazi kuwa TID ameshoot kwa camera ya simu.

Zaidi msikilize TID hapa chini.