Akiongea kupitia eNEWZ Ditto amesema kwa matatizo anayopata Chid, jamii inapaswa kuelewa na kufahama kwamba ni matatizo kama matatizo yeyote na yanaweza kumtokea mtu yeyote hivyo kila mtu anapaswa kumsaidia Chid na sio kumbeza.
''Naumia sana ninapoona kuna watu wanachukulia matatizo ya Chid kama sehemu ya kujinufaisha na kuyachukulia kwa njia ya kuyatangaza na kujionyesha kwa kile wanachokifanya, mtu kama anampango wa kumsaidia hapaswi kutangaza afanye vile anavyoona itakuwa inamuondolea tatizo" amesema Ditto.

Ditto pia ameweka wazi nia yake ya kuhakikisha anajaribu kwa upande wake kumsaidia Chid pale atakapoweza ila hajaweka wazi kwasasa kwamba atafanya jambo gani ambalo huenda likamsaidia Chid.
Chid Benz anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya zinasosadikiwa kuwa ni Heroine.

