Dokii aeleza sakata la Harmonize kumsaidia Mavoko

Jumatatu , 13th Jul , 2020

Baada ya maswali kuwa mengi kuhusiana na ukimya wa muda mrefu wa msanii Rich Mavoko, EATV & EA Radio Digital imepiga stori na Dada wa msanii huyo Dokii na amenyoosha maelezo kuhusu ukimya wa Mavoko na kusaidiwa na Harmonize.

Msanii Rich Mavoko upande wa kulia, kushoto ni dada yake Dokii

Kuhusu ukimya wa msanii Rich Mavoko Dokii ameeleza kuwa  "Hata kama haonekani wamuache atulie, kama kuna tatizo wao watamsaidia nini, waache wakisikia tatizo kuhusu Mavoko ndiyo waniulize ila kwa sasa kila kitu kipo sawa, waache wawe na shauku ya kumuona hadi pale atakapotoka kuna vitu vizuri vinakuja".

Aidha akizungumzia suala la Harmonize kutaka kumsaidia Rich Mavoko kupitia post aliyoweka katika mtandao wa Instagram siku kadhaa zilizopita, Dokii amesema "Ilikuwa ni jambo zuri kama limetoka moyoni mwake, ulikuwa ni ujumbe mzuri na niliufurahia kwa sababu anajua anachofanya, Harmonize hajafanya jambo baya".

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.