Alhamisi , 15th Oct , 2015

Star wa filamu Eddy Gathegi mwenye asili ya Kenya, ameendelea kuchana mawimbi kimataifa kwa upande wa uigizaji ambapo hivi karibuni ataanza kuonekana katika tamthilia kubwa ya muendelezo ya The Blacklist, katika awamu yake ya kwanza toleo la 3.

Nyota wa filamu kutoka nchini Kenya Eddy Gathegi

Eddy ambaye ndani yake anashiriki kama Mr. Solomon, akiwa anatarajiwa kuonesha uwezo wake na kufikia mashabiki wengi zaidi kupitia fani ya uigizaji, ambayo aliamua kujikita ndani yake akiweka pembeni mchezo wa mpira wa kikapu ambao alishindwa kuendelea nao baada ya kuumia vibaya.

Mbali na tamthilia hii mpya ya The Blacklist, Eddy pia amekwishatokea katika filamu na tamthilia kadhaa ikiwepo House, Gone Baby Gone, Twilight Saga: New Moon na X-Men.