EXCLUSIVE : Nandy aeleza mipango ya ndoa yake

Ijumaa , 17th Jan , 2020

Msanii wa kike anayefanya vizuri kutoka BongoFleva Nandy, amepiga stori na EATV & EA Radio Digital na kueleza mipango yake ya ndoa, pia amefunguka sababu zinazofanya wasanii wengi wa kike wasiingie kwenye ndoa.

Picha ya msanii Nandy

Kupitia post yake aliyoweka katika mtandao wa kijamii wa Instagram, Nandy ameandika anatarajia kuwa mke wa mtu ambapo ameeleza "Kila mwanamke anastahili ndoa, wakati wa Mungu ni wakati sahihi sijui nitaolewa na nani aidha msanii au la ila tuombeane uzima nitaingia huko mwaka huu au mwakani" amesema Nandy. 

Aidha akizungumzia kuhusu sababu zinazofanya wasanii wengi wa kike wasiingie kwenye ndoa, Nandy amesema wanawake wengi wanapanga mipango yao ya baadae kutokana na ratiba na kazi ambazo wako nazo.

"Sidhani kama sisi ni wagumu kuingia kwenye ndoa ila watu hawaingii kwenye viatu vyetu, hamjui ambayo yapo kwetu kuanzia ratiba, kazi ambazo tunazo sio kama hatuingii ila sababu ni kupanga mipango ya baadae ila siwezi kuwaongelea wengine kwa mimi sio muda mrefu nitaingia kwenye ndoa" ameeleza Nandy.