Jumatatu , 5th Jan , 2015

Msanii wa muziki Mwana FA, akiwa kama msanii mkongwe katika sanaa akijivunia mafanikio yake bila kuwa na skendo za hapa na pale.

msanii wa miondoko ya bongofleva Mwana Fa

FA amesema kuwa mtindo wa wasanii wa siku hizi kujitengenezea matukio ili kupata 'kiki' ya kazi zao za kimuziki, si mbaya endapo unawasaidia kufanikisha kazi zao.

Mwana FA ambaye yeye binafsi haamini katika kutengeneza matukio ili kufanikiwa kisanaa, ametoa busara zake na kusema kuwa kwa upande wake anaamini kila msanii ana nguvu na madhaifu yake na kitu cha kwanza kuzingatia katika sanaa ni kazi nzuri.