Jumatano , 11th Jun , 2014

Rapa Mwana FA, aka The Choir Master leo hii amejikuta akikaangwa na maswali kibao kutoka kwa mashabiki na wadau kutoka familia kubwa ya wapenzi wa ukurasa wa Facebook wa EATV, katika kipengele chake maarufu cha 'Kikaangoni Live'.

Msanii Mwana FA akichat na mashabiki

MwanaFA katika muda wa saa mbili amejibu maswali ambayo pia mengine yamekuwa ni msaada kwa kuonyesha njia kwa wale wote wanaomfuatilia, katika harakati zake za kila siku za kimaisha.

Baada ya Mwana FA, sasa macho yote yanaitazama wiki ijayo kwa hamu kubwa kufahamu atakuwepo staa gani kwa ajili ya kuchat nae LIVE, endelea kufuatilia, like na share na marafiki ukurasa huu wa www.facebook.com/eatv.tv kwa burudani kama hii na nyingine kali.