Jumatano , 21st Feb , 2018

Rapa Fid Q amesema kwamba wasanii wa Hip Hop wana kazi kubwa ya kuelimisha mashabiki kuwa wanaweza kubadilika na bado muziki wao ukawa bora zaidi na kuweza kwenda na alama za nyakati ili kuweza kuufanya mziki wa Hip Hop kuwa na soko kubwa zaidi.

Fid Q amesema hayo baada ya kupata maoni mengi ya kum-diss baada ya kutoa ngoma ya Fresh kwa madai ya kuwa amelegeza japokuwa ilikuwa na mvuto kwa baadhi ya mashabiki kitu ambacho amedai kuwa mashabiki wanapaswa kueleweshwa kwani sanaa inahitaji mabadiliko.

Fid Q amesema kwamba wasanii wa Hip Hop bongo hawajabadilika ila midundo ya hip hop ndiyo imebadilika hivyo wanaosema kwamba  wasanii wa hao wamekimbia muziki huo mwaka 2017 wanakosea.

Hata hivyo Fid amewasihi wasanii wa Hip Hop kuacha kuogopa kufanya mabadiliko katika muziki huo kwa kuogopa kwamba wataambiwa wamelegeza katika mashairi yao kwa kuwa hakuna mafanikio yoyote yatakayotokea katika muziki wa Hip Hop kama wasanii wenyewe hawata fanya mabadiliko kwa bidii.