Emmanuel Mbasha akiwa na Flora Mbasha kabla ya kuachana
Akiongea kupitia eNEWZ Flora ambaye amesema anataka kuitwa madam Flora kwa sasa kwa kuwa maisha yake anayoyaishi kwa sasa yana amani na furaha hivyo anapendelea kuishi vile apendavyo yeye na kwa sasa hapendi kuongelea kwenye media kwa kuwa maisha yake hayatawanufaisha chochote.
Hata hivyo Madam Flora amesema kwa sasa hajali watu wanayoyaongea juu ya maisha yake na Mbasha kwa kuwa wengi wanaoongea hawamfahamu na wala hawajawahi hata kumshika mkono lakini pia hakusita kumuombea Mbasha kuwa Mungu ampiganie.