Jumatano , 20th Mar , 2019

Msanii wa Bongo Fleva na muandishi wa nyimbo, Foby ametangaza rasmi kuacha kuandikia wasanii nyimbo mpaka kuwe na mkataba maalumu ambao utaleta faida kwake na hii ni  baada ya wasanii wengi kumsumbua akiwemo Hamisa Mobetto.

Foby na Hamisa Mobetto

Fobby anasema kwamba amekuwa akikutana na changamoto nyingi pale alipokuwa akiwaandikia wasanii nyimbo lakini wasanii wameshidwa kumshukuru wala kumthamini baada ya nyimbo hizo kufikia malengo na kupata umaarufu hivyo kwa sasa anaandika nyimbo kwa mikataba na makubaliano maalumu ili kuepusha lawama baina yake na msanii anayemuandikia.

"Mimi nimemuomba Hamisa Mobetto tufanye wimbo ya pamoja kwa maana kwamba nilimuomba kumshirikisha lakini hakuwa tayari kabisa kiasi kwamba hata 'sms' alikuwa ananijibu baada ya siku tano tofauti na yeye alivyokuwa akitaka nimtungie nyimbo alikuwa anajibu 'sms' zote kwa wakati kitu ambacho kimenishangaza sana", amesema Foby. 

Hata hivyo Foby amesema kwamba yeye ni mtu ambaye alimsaidia Hamisa kujua kuimba kwa kuwa wakati anakuja kwake alikuwa hajui kufanya kitu chochote na clip zote ambazo zinaonyesha yeye akimfundisha Hamisa kuimba anazo ila kwa sasa anashangaa akimuomba kolabo msanii huyo anaambiwa asubiri afikirie kwanza kitu ambacho kimemvuruga na kumtia hasira.

Bonyeza hapa chini kutazama zaidi.