Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Godzilla amkana mpenzi wake

Jumatatu , 21st Aug , 2017

Rapa Godzilla ambaye kwa sasa anasumbua na ngoma ya  'X ' amekanusha kuchanganyikiwa kutokana na kuachana na mpenzi wake na kudai kuwa yeye siyo wa kwanza kushindwa kufika mbali na mpenzi wake na kwamba maneno yanaletwa na umaarufu wake.

Rapa Godzilla

Akizungumza na mwandishi wetu Godzilla amesema kwamba watu walikuwa wanamuona kama kachanganyikiwa kutokana na kutokujua ni nini kilichokuwa kinaendelea kwenye maisha yake hivyo wengi walikuwa wakimchokonoa ili kuweza kumfahamu zaidi kutokana tu tayari yeye ni msanii lakini pia siyo mtu wa kuonyesha maisha yake binafsi hadharani.

"Nashangaa hata hayo maneno yalipokuwa yanatoka, lakini kwa vile mimi ni maarufu lazima mishale inayorushwa kwangu mingine inipate hivyo kwa kuwa hilo nimeshalifahamu ndiyo maana nimekuwa kimya kwa sababu sipendi maisha yangu kuwa wazi kwa kila mtu. Unajua kuna mtu anaishi Temeke lakini ukimkuta anasimulia maisha yangu ya Salasala utadhani ananijua sana lakini siwezi kuwajibu tayari mimi ni msanii hivyo napokea mishale yao" Zilla

"Ni kweli nilikuwa kimya watu wakaanza kuni attack pasipokujua mimi nafanya nini. Nilikuwa nashughulika na studio yangu kukamilika na tayari tumeshamaliza hilo. Kila kinachohitajika ndani ya studio tumeshanunua na kazi zitaanza kusikika na vitu vingi ambavyo tutakuwa tunatengeneza hapo vitaanza kusikika na kuonekana hivi karibuni".

Akizungumzia kuhusu wimbo wa 'X'  Zillah amesema kuwa hakumlenga mtu yeyote kwenye wimbo huo na badala yake ni kama kutoa ujumbe kwa mtu anayetaka mafanikio lazima kufuta baadhi ya watu wanaomfanya mtu asifanikiwe.

"Sijamlenga aliyekuwa mpenzi wangu kwenye wimbo huu. Mimi ni msanii natakiwa kuburudisha watu. Kwenye wimbo huu maisha yangu sijayaweka lakini ni ujumbe ambao nimeufikisha mtaani kuwasaidia watu wanaohitaji kufanikiwa katika maisha na ndiyo maana ya 'X',  Siyo lazima ung'ang'ane na watu ambao hawakufanyi wewe upate mafanikio" Zilla aliongeza

Zilla ameahidi kuachia kichupa cha wimbo huu haraka baada ya kuitambulisha 'Audio' mapema wiki iliyopita.

HABARI ZAIDI

Bujukano Mahungu John, Mwenyekiti wa Umoja wa Waganga na Wakunga wa Tiba Asili Tanzania

Waganga wa jadi waungana kukemea ukatili, Geita

Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Mvua zilizoambatana na upepo zimeua watu watano TZ

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP