Kwa mujibu wa orodha ya International Federation of the Phonographic Industry (IFPI) kupitia ripoti yake ya IFPI Global Artist Chart, Drake ameendelea kuongoza kwa mauzo, streams na ushawishi mkubwa katika soko la muziki duniani.
Mafanikio haya yanaonesha uimara wake katika tasnia ya muziki, hasa katika enzi ya streaming ambapo ushindani ni mkubwa zaidi kuliko wakati wowote ule. Tangu alipoanza kupata mafanikio makubwa mwanzoni mwa miaka ya 2010, Drake amekuwa akivunja rekodi mara kwa mara kupitia albamu na nyimbo zake zinazoongoza kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki.
Katika kipindi cha miaka 11, amewashinda wasanii wengi wakubwa wa hip hop na muziki kwa ujumla, jambo linaloonesha uwezo wake wa kubaki kileleni kwa muda mrefu.Wachambuzi wa muziki wanasema siri ya mafanikio yake ni uwezo wa kubadilika kulingana na mabadiliko ya soko, pamoja na kuwa na mashabiki wa kudumu duniani kote.
Drake anaendelea kuthibitisha kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii wakubwa zaidi katika historia ya hip hop ya kizazi hiki.




