Hamisa Mobetto ahofia kupigwa

Jumatatu , 3rd Jun , 2019

Siku za hivi karibuni mwanamitindo ambaye pia ni mwimbaji Hamisa Mobetto, amekuwa karibu na msemaji wa klabu ya Simba na wamekuwa wakionekana kuwa pamoja kwenye mambo mbalimbali ikiweko uwanjani.

Hamisa Mobetto

Ukaribu huo umezua maswali mengi huku Hamisa mwenyewe akionekana anahofia kupigwa kutokana na ukaribu huo, ambapo ameeleza hofu hiyo kupitia post ya Manara kwenye mtandao wa Instagram iliyowaonesha wakiwa pamoja.

Manara alipandisha picha hiyo Jumapili Juni 2, 2019 na kuandika hivi ''Team Samata tushampiga Kiba Sita na baadae tunafuturu kichanpioni Serena hotel''. Hamisa baadae alicomment na kuandika, ''Ipo siku utafanya tupigwe''.

 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

Team Samata tushanpiga Kiba Sita na baadae tunafuturu kichanpioni Serena hotel @hamisamobetto

A post shared by Haji S. Manara (@hajismanara) on

Manara na Hamisa ambaye pia ni shabiki wa Simba, walikaa pamoja uwanja wa taifa na kutazama mechi ya Simba dhidi ya TP Mazembe na ile ya Simba dhidi ya Sevilla huku Manara akiweka picha zao mtandaoni.