Harmonize feki achezea kichapo kisa Mwanamke

Jumatatu , 23rd Mar , 2020

Moja kati ya video inayozunguka kwa sasa mitandaoni, inamuonesha jamaa mmoja akichezea kichapo kutoka kwa mwanamke aliyemdanganya kuwa yeye ni Harmonize wakati sio kweli ili mradi awe naye kwenye mahusiano.

Picha ya Harmonize feki

Jamaa huyo ambaye jina lake halijajulikana, amechezea kichapo hicho mbele ya waandishi wa habari huku mwanamke huyo akiwa amemkunja shingoni, huku akimuuliza kwanini amemdanganya kuwa yeye ni Harmonize katika mtandao wa Instgram.

Katika utetezi wa jamaa huyo alisikika akisema "Muonekano ni kama hivi unavyouona ni fresh tu, mimi nafanana na Harmonize sijifananishi bali nafananishwa na watu ausio ila nampenda sana".

Aidha wakati huo mwanamke huyo alikuwa anampiga kichwani huku amemkunja na kumuuliza  "Kwanza usiniguse wewe una Corona, ongea vizuri kwanini umeamua kunidanganya wewe ni Harmonize na ukanitongoza Instagram".