
Jaguar
Jaguar ameonekana hivyo kupitia picha aliyopost katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuandika "Habari za asubuhi kutokea Dar Es Salaam".
Jaguar kwa sasa yupo nje kwa dhamana baada ya kusota jela kwa wiki kadhaa zilizopita, kwa kosa la kutoa lugha za kichochezi , na maneno ya chuki kwa wageni na watanzania ambao wanaishi nchini Kenya.
Aidha baada ya kutoa kauli hizo na kuwekwa jela, Jaguar mwenyewe amekuwa akikataa kwa kusema watu hawakumuelewa vizuri na wala hakuwa na nia ya kuwafukuza wageni na wala hana shida yoyote na watanzania waishio nchini Kenya.