Jumatatu , 29th Jul , 2019

Msanii na mtayarishaji wa muziki Nahreel, Leo ametueleza upande wa pili wa maisha yake mbali na kazi ya usanii na utayarishaji ambayo anaifanya kwa sasa.

Nahreel ameeleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital baada ya kuulizwa kama mbali na muziki kitu gani kingine anachokifanya, “Mimi nilianza kucheza mpira kabla sijaanza masuala ya uandaaji na usanii, kipaji nilichoanza kukigundua ni mpira wa miguu, na nilianza
kucheza mpira wa miguu kuanzia shule ya msingi hadi sekondari lakini baada ya hapo muziki ndio ukaingia

Aidha msanii huyo ameongeza kwa kusema anapenda sana mpira na tangu mwaka huu uanze kila siku anafanya mazoezi na anapendelea kucheza nafasi ya mshambuliaji na beki wa kati, timu anayoipenda na kuishabikia ni FC Barcelona.

Nahreel anaungana na mastaa wengine kama Ali Kiba, Tunda Man ambao waliwahi kusema kama isingekuwa muziki wangekuwa wanasoka, Pia ametaja watayarishaji anaowakubali ni S2Kizzy, Abbah, pamoja na Black.