Jumanne , 21st Apr , 2026

Mtangazaji wa kipindi cha madini dot com grayson gideon amefunguka kuwa msanii ibraah ni msanii mwenye kipaji kikubwa na uwezo wake ni mkubwa sana kwenye uandishi na vitu vingine vingi vinavyomkamilisha msanii Chinga anavimiliki.

Ameendelea kwa kusema kuwa kama kuna mdau ambaye anataka kuwekeza kwa msanii huyu basi atakuwa amefanya jambo ambalo hatajutia kwenye uwekezaji wake.
 

Kwenye ukurasa wake wa Instagram Grayson ameandika...........1.Sauti ya mkwaruzo ✅
2. Uandishi kuntu ✅
3.Kuongeza thamani kwenye Collabo za wengine✅
4.Uwezo wa kufanya HIT kwa topics na genre tofauti ✅
4.Personality na experience ya Ustaa wa mainstream✅
5.Story ya maisha binafsi na ya mziki inayouzika ✅

Kitu pekee ibraah anahitaji kuchunga ni namna anavyodeal na watu kiujumla nje ya music(Tabia binafsi) akipata mwongozo anavyodeal na Dunia yake, hakuna cha kumzuia Chinga kwenye BONGOFLEVA hii na ijayo.Vijana wengi wenye Talent kubwa huathiriwa na pale TABIA BINAFSI zinakuwa hazisapoti UWEZO BINAFSI, sio Kwa namna mbaya, hata tabia positive Zinaweza kuwa HAZINA msaada na talenti, huo mwongozo tu, lakini kimuziki stoku ya HITSONGS kwenye uwezo CHINGA ni unkwepekabo thing tuendako.This is how wetalkMusic.