Alhamisi , 14th Jan , 2016

Nyota wa muziki Inspekta Haroun 'Babu' ambaye yupo katika game ya muziki kwa muda sasa, amekuwa ni kati ya wasanii ambao wameamua kwenda sawa na kasi ya mabadiliko katika game ya muziki haswa katika kizazi hiki cha sasa.

Nyota wa muziki nchini Inspekta Haroun 'Babu'

Babu amesema kuwa safari zake Afrika Kusini zinakuwa ni moja kati ya jitihada kuhakikisha kuwa licha ya ukongwe katika fani, hapitwi na muda.

Inspekta amesema kuwa, kutokana na fursa nyingi za kupiga hatua kimataifa kupatikana Afrika Kusini, amekuwa nchini huko kujifunza mambo mengi kati ya hayo, kutokana na kutaka muziki wake kufika mbali zaidi ya alipoweza kuufikisha sasa.