Ijumaa , 11th Jul , 2014

Baada ya kutoa wimbo wake mpya ambao umetambulishwa wiki hii uliobatizwa jina 'Walala Hoi' msanii Izzo Bizness aamua kuweka wazi kuhusiana na swala zima la kufanya kolabo na kushoot videos na wasanii nchini.

Msanii wa bongo fleva Izzo Bizness

Izzo Bizness ameongea na enewz juu ya zoezi hilo haswa ukizingatia asilimia kubwa ya wasanii nchini huchaji kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kufanya colabo na kazi zingine za muziki.