
Kushoto ni Dogo Janja, kulia ni Young Dee
Jambo hilo limetokea kwenye mtandao wa Instagram baada ya Dogo Janja kushea 'EP' ya Young Dee huku akimnyooshea mikono juu kwa kumwita mfalme wa wasanii wote wa kizazi hiki cha vijana.
"Kati ya watu niliokutana nao ambao ni Walimu, huyu chalii Youngdaresalama yumo! bonge la EP kamanda, Mfalme wa Young Generation" ameandika Dogo Janja
Baada ya Post hiyo rapa Young Dee akajibu kwa kuandika kuwa "Young King thanks mwanangu"
Kwa kauli hizo inaashiria kuwa hakuna tofauti yoyote kati ya wasanii yao na wamemaliza utata wa muda mrefu uliosemeakana kwamba wasanii hao hawana stori wala maelewano mazuri.