Jumatatu , 22nd Feb , 2016

Mtindo wa kutafuta kiki kwa wasanii ili kuingiza kazi zao mpya sokoni umechukua sura mpya, hili likiwa limegundulika na eNewz baada ya kufuatilia kwa undani beef inayotajwa kuwepo kati ya msanii Dogo Janja na uongozi wa TIP TOP.

DOGO JANJA NA MADEE

Hivi karibuni ilivuja sauti ya Dogo Janja akiongea kwa simu na girlfriend wake ambapo alisikika akiukashifu uongozi wa TIP TOP kuwa umekuwa ukiua vipaji vya wasanii wa TI TOP akiwemo yeye.

Kwa mujibu wa maelezo ya Dogo Janja anadai sauti hiyo ilirekodiwa bila yeye kufahamu akiwa anajaribu kumuingiza katika nyavu zake girlfriend wake, baada ya msichana huyo kumuuliza Dogo Janja sababu za kupotea katika ramani ya muziki.

Kwa upande wa Madee ambaye ni msimamizi wa msanii huyo, ametoa kauli ya utata kuwa anazielewa hisia za Dogo Janja, wakati huo huo, ikionekana kuwa wapo pamoja wanafanya kazi mpya ingawa anakana kukutana na kuzungumza na msanii huyo kuyaweka mambo sawa baada ya hitilafu hizo kujitokeza.