Jumatatu , 10th Nov , 2014

Baada ya kufanya kolabo na wasanii mahiri wa Hip Hop nchini katika wimbo wa 'Kupanda na Kushuka' mWanamuziki nyota Lady Jadee hivi sasa ajipanga kufanya wimbo na mdogo wake ambaye ni mkali wa miondoko ya reggae na dancehall Dabo.

wasanii lady Jaydee na mdogo wake Dabo

Jide aka Commando ameelezea kuwa wimbo huo mpya alioubatiza jina 'Forever' utakuwa ni wimbo wake wa kwanza kuuimba kwa kushirikiana na Dabo ambaye ni mdogo wake anayemfuata baada ya kuzaliwa yeye.

Wimbo huo mpya unatarajiwa kukamilika kuanzia tarehe 28 ya mwezi Novemba mwaka huu.