Jumamosi , 17th Apr , 2021

Shabiki na Mwanachama wa Klabu ya Yanga Jimmy Kindoki amempa onyo msanii wa singeli Dulla Makabila ambaye ametangaza kuihama timu hiyo na kuhamia Simba kwa kusema hataki kumuona tena akirudi kwani amefanya kitendo cha usaliti kama Yuda.

Kushoto ni Jimmy Kindoki, kulia ni msanii Dulla Makabile

"Ole wako tusikie umerudi Yanga ndio utajua siku hiyo kama Yanga inawenyewe, mmekosa kiki kwenye muziki wenu sasa mnahamia huku, nikwambie tu hiyo furaha ya Simba ni ya muda mfupi siku huyo Moo akisema basi ujue Simba inarudi kwenye msoto"

"Halafu tukusike unaleta kiherehere chako baki huko huko uliposema unahamia huku hatuhitaji wasanii wasiojielewa na kwa kiongozi yoyote atakaemkaribisha huyu Yuda kwenye hafla za Yanga hatutaelewana" ameeleza Jimmy Kindoki

Siku chache zilizopita msanii Dulla Makabila aliweka taarifa ya kuihama timu yake ya Yanga kutokana na matokeo mabovu wanayoyapata kwenye baadhi ya michezo yao ya siku za hivi karibuni.