Jinsi wasanii walivyompa mashavu JK

Jumatatu , 7th Oct , 2019

Leo Oktoba 7 miaka 69 iliyopita, alizaliwa kiongozi mahiri na shupavu, ambaye ni Rais mstaafu wa Awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.

Dkt Jkaya Mrisho Kikwete, aliliongoza Taifa la Tanzania kwa kipindi cha miaka 10, kuanzia mwaka 2005 hadi 2015, kisha kumuachia kiti hicho Rais wa sasa Dkt  John Pombe Magufuli.

Wasanii na watu mashuhuri nchini, kupitia kurasa zao mbalimbali za mitandao ya kijamii wamemuandikia jumbe za kumtakia heri ya kuongeza umri mwingine kwenye maisha yake.

Hii ni orodha ya mastaa na watu maarufu waliompost Rais huyo mstaafu, kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Jacqueline Wolper “Mshua Bwaaana unapendwa paka nawasiojua kuongea, Mungu akuweke we love u so Much ,? happy birthday Dady @jakayakikwete ”

Wema Sepetu “Libra President...!!! The King of The Jungle...!!! Happy Birthday to You...!!! We Celebrate You today”

Ommy Dimpoz “Heri ya kuzaliwa Mzee Wangu JK @jakayakikwete Allaah Azidi kuimarisha Afya yako, Akupe Umri Mrefu Inshaallaah Kwani Hekima na Busara zako bado zinahitajika”

Duma Actor “ Happy birthday Dady !!!!“

Mc Pilipili “Happy Birthday Baba @jakayakikwete “

Mastaa wengine waliopata bahati ya kuzaliwa siku moja na Dkt Kikwete ni waigizaji wa filamu nchini Tanzania ambao ni Rosse Ndauka , Rammy Gallis na Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga Jerson Tegete.