Jux amjibu Mimi Mars "Mapenzi sio mashindano"

Jumatano , 4th Dec , 2019

Mkali wa muziki wa RnB Juma Jux, amemjibu Mimi Mars kwa kumwambia mapenzi sio mashindano, baada ya msanii huyo wa kike kusema dada yake Vanessa Mdee amempata mtu wa level zake ambaye ni  muigizaji wa filamu aitwaye Rotimi.

Kushoto kwenye picha ni Jux na upande wa kulia ni Mimi Mars

Jux amesema hivyo kupitia EATV & EA Radio Digital, ambapo ameeleza kuwa mapenzi sio mashindano na mtu unatakiwa kufanya kutokea moyoni.

"Sijui kwanini amesema hivyo ila kama ni yeye ameona hivyo sawa siwezi kukataa, kwanza muda huo sina pili mimi nina maisha mengine, pia ninaheshimu mawazo yake hata kama anaona hivyo lakini ninachoweza kusema kwenye maisha ya mapenzi hakunaga mashindano" ameeleza.

Aidha Jux ameendeleza kusema "Kwenye mapenzi hutakiwi kufanya kwa mashindano inabidi ufanye kutoka moyoni mwako  na mtu unayempenda, inabidi uhakikishe uwe na  mtu ambaye ni wa ukweli, usiwe naye kwa sababu ya fulani" ameongeza.

Mapenzi ya Jux na Vanessa Mdee yalikuwa yanaushawishi kwa watu wengi pia yalidumu kwa miaka mitano, sasa hivi kila mtu ameanzisha mahusiano yake mapya  ambapo Jux anatoka na mrembo Nnayika, huku Vanessa yupo penzini na Rotimi.