Jumatano , 18th Mar , 2020

Baada ya kuwepo na taarifa za kuwa wapenzi kati ya msanii wa Tanzania Juma Jux dhidi ya mrembo na mwanamitandao Huddah The Bosschick, huenda zikawa za ukweli kwa sababu ukaribu wao unaongezeka kila kukicha.

Juma Jux na Huddah The Bosschick

Suala hilo limethibitika kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram ambapo Jux amepost picha kisha Huddah akaja ku-comment kwa kuandika  "Yaani sasa hivi Zanzibar ni sehemu bora ya kukaa rafiki yangu, nitakuona huko".

Baada ya mrembo Huddah kuachia comment hiyo, Jux naye akamjibu kwa kuandika  "Kabisa rafiki yangu ahsante kwa kuniongezea mwanga rafiki yangu".

Ikumbukwe tu taarifa za wawili hao kuwa na uhusiano zilinza kuripotiwa tangu walipoonekana wapo katika hoteli moja huko visiwani Zanzibar, ambapo kila mtu alienda kupumzika kivyake.