"Kaka Tuchati haizidi elfu 60" - Stamina 

Jumamosi , 16th Mei , 2020

Msanii wa HipHop kutoka kundi la Rostam Stamina amesema video ya wimbo wao mpya "kaka tuchati" imewagahrimu kiasi cha shilingi elfu 60.

Roma na Stamina, kwa pamoja wanaunda kundi la Rostam

Akizungumza kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa TV, Stamina amesema idea ya video ya wimbo huo umetoka kwa Director Nicklass ambaye awali aliwaambia anataka kufanya kazi hiyo kila mtu akiwa kwake, pia video hiyo imeshutiwa kwa njia ya simu na sio camera kama ilivyozoeleka.

"Hii video haina bajeti yoyote haizidi elfu 60, gharama nilizozipata ni kuweka bundle na kudownload zile clip, na video yetu haijashutiwa na Camera" amesema Stamina