Jumatano , 4th Feb , 2015

Rapa Kala Jeremiah, ameweka wazi mtazamo wake tofauti kuhusu suala la wasanii hapa Tanzania kufanya kolabo na wasanii wa nje ili kwenda kimataifa, na kusema kuwa njia nzuri zaidi ya kufanikiwa hivi ni kujikita hapa nyumbani Tanzania.

Msanii wa muziki wa bongofleva nchini Kala Jeremiah

Kala amesema kuwa kujikita hapa nchini ni kwa sababu kuna soko kubwa ambalo hawajaweza kulifikia hata robo yake.

Kala amesema haya akitolea mfano wa badhi ya wasanii wa Uganda ambao wameweza kujitengenezea utajiri mkubwa kwa kufanya kazi ndani ya nchi yao pekee, ikiwa ni kama wito kwa wasanii kujiboresha na kulitumia zaidi soko na mashabiki wa nyumbani kabla ya kutoka nje.