Ijumaa , 27th Feb , 2015

Wachekeshaji mahiri wa Afrika, Anne Kansiime kutoka Uganda na Bascket Mouth kutoka Nigeria wamepata shavu la kusherehesha tukio la ugawaji tuzo za Africa Muziki Magazine, zitakazofanyika mwezi wa 10 nchini Marekani.

Anne Kansiime | Bascketmouth

Uteuzi wa wakali hawa wa kuvunja mbavu, tayari umeongeza msisimko mkubwa kwa wapenzi wa burudani kutokana na uwezo wao mkubwa katika fani hiyo.

Africa Muzik Magazine Awards ama AFRIMMA, ni tuzo zinazoandaliwa huko Marekani, kwaajili ya kutambua sanaa ya muziki wa kiafrika kwa ujumla.