"Kata ya Mwanga Kaskazini ni yangu binafsi" - Baba

Jumatano , 29th Jul , 2020

Ni habari kutoka kwa msanii Baba Levo ambaye amesema, wajumbe wameshamaliza kazi baada ya kushinda kura za maoni kwa asilimia 97 ili aweze kuwania Udiwani wa Kata ya Mwanga Kaskazini, Kigoma kupitia chama cha ACT Wazalendo.

Msanii Baba Levo

Kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kushinda kura za maoni Baba Levo ameeleza kuwa, atakayekuja kushindana naye bora aache kwani Kata ya Mwanga Kaskazini ni kata yake binafsi.

"Nashukuru chama changu cha ACT Wazalendo na Wajumbe kwa kunipa ridhaa na nafasi ya kuchukua fomu ya Udiwani, anayekuja kugombea Udiwani na mimi anatakiwa kujua kuna mwenyewe na Mwanga Kaskazini ni Kata yangu binafsi, waache kujisumbua na kupoteza pesa, tena bora hiyo pesa angeanzisha biashara hata ya vikoba kwa sababu kuniangusha haiwezekani" ameeleza Baba Levo.

Zaidi tazama mahojiano kamili hapa chini.