
Godfrey Mngereza wa pili kutoka kushoto, baada ya kufanya interview kwenye kipindi cha PlanetBongo
Taarifa hizo zimethibitishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya BASATA ambaye ametangaza kifo hicho na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi ambapo ameshea ujumbe wa mwisho aliotumiwa na Godfrey Mngereza kabla ya kufariki.
"Nimelazwa General hapa Dom ila kila kitu kitaenda sawa kuhusu tamasha napambana, ni meseji ya mwisho niliyoipokea juzi Jumanne saa tano na dakika 2 usiku kutoka kwa kaka yangu Godfrey Mungereza, Katibu Mtendaji wa BASATA, leo hatunaye tena katika dunia hii ametutoka, tumuombee sana mola ampe pumziko la amani la milele" ameandika Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi
Ratiba ya mazishi bado haijatolewa ila tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu kukupa kile kinachoendelea kuhusiana na msiba huu.